Last update: 2010-10-28

MAHOJIANO YA DR. SLAA NA ITV YALIYOBADILISHA MWELEKEO!

play
2010-10-28 Length: 1h 48m 14s

Dr. Slaa alipata nafasi ya kuzungumza siku ya Jumamosi na kituo cha Televisheni cha ITV kuhusu masuala mbalimbali ya kampeni na mwelekeo wake wa uchaguzi. Matangazo hayo yalichangia kwa kiasi kikubwa kubadilisha mawazo ya watu mbalimbali kuhusu Dr. Slaa na kumpatia mashabiki wengine wengi. Hata hivyo marudio ya kipindi hicho tumedokezwa yamepigwa marufuku... Hii ni nafasi ya kuyasikiliza kwa wale ambao hawakupata nafasi. …


Exclusive: Mahojianona Fred Mpendazoe - Mbunge aliyeikacha CCM na kujiunga CCJ!

play
2010-04-11 Length: 28m 39s

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapmduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani; wala,dalili zozote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasi wasi! - Nyerere Watanzania bado wana maswali juu ya Chama Cha Jamii (CCJ) hasa kama kweli hiki chama kimekuja kuziba pengo la uongozi nchini au ni geresha tu kama ya vyama vingine. Kabla hata ya kwenda kuomba usajili wa muda tetesi zilishasambaa juu ya ujio wa chama hicho na ndani ya wiki chache tu CCJ kimepata kutangazwa sehemu mbalimbali kwa bure kabisa huku kikivuta mioyo ya wananchi wa kawaida kabisa waliochosha na vyama vya kisiasa vilivyopo ambao kwa muda mrefu wamesubiria kuona matamanio ya Baba wa Taifa kuhusu chama mbadala cha upinzani yakitimia. Tetesi kubwa ni uwepo wa vigogo nyuma ya CCJ na wapo ambao hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe au kufikiri wenyewe kuhusu CCJ hadi waone kwanza nani ameondoka CCM. Kwa wale ambao wanasubiri wasikie “majina makubwa” yakitoka CCM ndio waamini basi kutoka kwa Bw. Fred Mpendazoe hakuwatoshi. Ni wazi vile vile hata likitoka kundi jingine ndani ya CCM bado wapo watu ambao hawataamini na wataendelea kutafutua ufafanuzi kwanini hao siyo “vigogo” au kwanini kuondoka kwao “ni nafuu kwa CCM”. Vyovyote vile ilivyo, Watanzania wana haki na sababu ya kuipima CCJ kwa katiba yake, malengo yake, mapendekezo yake ya kushughulikia masuala ya taifa na itikadi yake. Itakuwa ni upungufu wa hekima, na uwezo wa kufikiri kama tutajaribu kukipima CCJ kwa kuangalia nani “anatoka CCM”! Mtu mwenye hekima atachukua muda kusikiliza kile ambacho uongozi wa CCJ, mashabiki wake, Katiba na watunga sera wake wanasema juu yake na siyo kile ambacho waathirika wa uwepo wa CCJ wanasema juu yake. Hivyo, mahojiano haya ya kwanza na Mhe. Fred Mpendazoe aliyekuwa Mbunge wa CCM wa kuchaguliwa kwa asilimia 81 (kura 64,000) na ambaye ameamua kuondoka CCM “mapema” yatatupa mwanga wa ni watu gani wako nyuma ya CCJ na kama tunaweza kukubali na kukumbatia uwepo wake katika kuendeleza demokrasia nchini na hasa katika kupatia uongozi “bora” ambao taifa limekuwa likiutamani na kuungojea kwa muda mrefu hasa baada ya kukatishwa tamaa na uongozi ulioingia 2005. Sikiliza na uamue mwenyewe. …


Mchango wa mjadala wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi; Ni sheria mbaya!

play
2010-03-04 Length: 18m 46s

Mapema leo nimeshiriki kwenye mjadala wa Star TV kuhusu sheria iliyopitishwa hivi karibuni ambayo inalengo la kusimamia matumizi ya fedha katika Uchaguzi. Rais Kikwete alitumia hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari kuelezea juu ya uzuri wa sheria hii na kwanini ataitia sahihi kwa mbwembwe kuonesha kuwa anatimiza ahadi yake ya 2005. Kwa maoni yangu sheria hii ni miongoni mwa sheria mbaya na ambayo itatuletea matatizo kuliko Sheria ya Madini ya 1998, Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya 1998 au Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1996. Sikiliza sehemu ya mchango wangu kwenye mjadala huo. …


Mahojiano na Waziri Phillip Marmo Juu ya Wagombea Binafsi

play
2010-03-02 Length: 25m 13s

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Bw. Phillip Marmo (pichani) amesema kuwa serikali haitokaidi uamuzi wa Mahakama kuhusu suala la wagombea binafsi endapo Mahakama ya Rufani itasisitiza kuwa waruhusiwe kwenye uchaguzi mkuu ujao kama ilivyoamuriwa na Mahakama Kuu mwaka 2005. Hata hivyo, Bw. Marmo amesema kuwa kutokana na mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mkuu kufikia mbali endapo msimamo wa mahakama utakuwa ni ule ule basi itabidi uchaguzi mkuu uahirishwe ili kuruhusu utaratibu wa kubadili Katiba na kuwezesha wagombe huru na binafsi kushiriki kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu. Pamoja na hilo Bw. Marmo amedokeza kuwa endapo itabidi Katiba ibadilishwe basi kuna uwezekano kuwa suala la mgombea binafsi litarudishwa kwa wananchi ili liamuliwe kwa kupitia kura za maoni. Akizungumza na KLHN International ambacho ni kituo cha Watanzania kirushacho matango kupitia mtandao wa Intaneti Bw. Marmo alisema kuwa hata hivyo kwa wakati huu suala la kura za maoni halipo “kwani tutavuka huo mto tukiufikia”. Kuhusu kile ambacho kinaonekana kuwa ni mgongano kati ya serikali na mahakama kuhusu suala la mgombea binafsi Bw. Marmo alisema kuwa hakuna mgongano wowote isipokuwa hivi sasa haupo muda wa kutekeleza uamuzi wa mahakama akidai kuwa rufaa iliyokatwa na serikali ilisababisha uamuzi wa awali usitekelezeke. Bw. Marmo alitumia mfano wa adhabu ya kifo ambapo rufaa ikikatwa basi adhabu ya awali ya kunyongwa haitekelezwi hadi rufaa iamuliwe. Hata hivyo alipoulizwa kwa kutumia mfano wa kesi ya Nalaila Kiula (aliyekuwa Waziri wa Ujenzi) na ile ya kina Nguza Viking ambapo wote licha ya kukata rufaa bado waliendelea kutumia adhabu zao Bw. Marmo alidai kuwa “kesi hizo ni za mazingira tofauti”. …


Mahojiano ya Mwanakijiji na PowerBreakfast - Clouds FM

play
2010-01-13 Length: 20m 22s

Nimepata nafasi ya kuzungumza kwa muda mrefu na mojawapo ya vipindi maarufu nchini Tanzania kile cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds FM. Nilizungumza na Bw. Gerald Hando. Hii ni sehemu ya mahojiano hayo. …


Mahojiano na Chama cha Msalaba Mwekundu na Mpango wa kusaidia wahanga wa Mafuriko!

play
2010-01-09 Length: 23m 0s

Unaweza kupata mpango tulio nao hadi hivi sasa wa kushiriki katika kuchangia wahanga wa mafuriko yanayoendelea nchini kupitia Chama cha Msalaba Mwekundu. Tumepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Mkuu wa Kitengo cha Maafa wa chama hicho nchini Bw. Joseph Kimaryo ambaye anatueleza hali ilivyo hadi hivi sasa (Jumamosi Januari 9, 2010). Kwa kushirikiana na tovuti za Jamiiforums na Mdau wa Jamii Bw. Issa Michuzi; pamoja na kushirikiana na Mtandao wa Wanaataluma wa Tanzania (TPN) tumeandaa mpango wa kuwashirikisha Watanzania mahali popote pale walipo kuchangia katika adha hii inayowakuta ndugu zetu katika mikoa mbalimbali hasa Morogoro, Dodoma, na sasa hivi Shinyanga na hata Mwanza na kuna uwezekano wa sehemu nyingine nchini kwa kadiri siku zinavyoendelea. Tumeamua kutumia Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania kwani rekodi yao katika kufika na kutoa misaada wakati wa majanga hailinganishwi na chombo au taasisi nyingine yoyote. Zaidi ya yote tumepata uhakika wa kutosha wa misaada yetu kufika kwa walengwa baada ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mstahiki Meya (Dar) Adam Kimbisa (CCM). Pata nakala ya mpango huo hapa: http://www.box.net/shared/g99no7hjkg …


Agenda 2010

play
2010-01-03 Length: 2m 30s

Ningeweza kutumia maneno mengi kuelezea kosa hili ambalo hata hivi sasa bado tunalifanya lakini hatuna budi kujisahihisha kama mabadiliko tunayoyataka yataweza kupata nafasi yoyote. Kosa hilo ni kosa ambalo hatujaona ubaya wake na ni nafasi hii kutafakari kama kuendelea nalo tunaendelea kujihukumu sisi wenyewe na uzao wetu kwenye utegemezi na uombaomba wa kudumu. Kosa tulilolifanya ni Kuwaachia wanasiasa wetu kuendelea kutengeneza ajenda za kisiasa kwa taifa letu na kutuletea sisi wananchi; tumewaacha waandike ilani zao na kutuletea sisi; tumewaacha wao waamue nini tunataka halafu wanatuomba kura kwa msingi huo.. Nasema sasa yatosha; 2010 "sisi wananchi wa Tanzania mahali popote tulipo na katika hali zetu zote tulizonazo, tutaamua tunataka nini, lini, na kwa namna gani; tutauza ajenda hiyo kwa wanasiasa wetu na ni kwa msingi huo ndio tutawachagua". Sijali tena CCM itaahidi nini; sijali CUF wataahidi nini; sijali Chadema wataahidi nini au watakuja na ilani gani. Wakati huu wao ndio watagombania kile tunachokitaka ili watuletee kwa namna tunayotaka. Kwa maneno mengine, hatima ya kisiasa na kiuongozi ya nchi yetu tunataka kurudisha mikononi mwa wananchi wenyewe. …


CCM matatani; Upinzani Mashakani - ngoma 2010!

play
2009-08-23 Length: 17m 49s

Sijui kama kweli tunataka mabadiliko au tunaombea mabadiliko yatokee. Sijui kama tunafanya ili kusababisha mabadiliko au tunasubiri wengine wafanye ili tufurahie mabadiliko; Sijui hata kama tunajua vizuri ni mabadiliko gani hasa tunayataka na kama tunataka ni juhudi gani tumezifanya kushiriki kwenye mchakato wa kuleta mabadiliko hayo.

Tunaweza kubishana vijiweni na kwenye mitandao na kujaribu kubadilishana mawazo mchana kutwa na usiku kucha lakini mabadiliko hayaji kwa kusema. Mabadiliko hayaji kwa kupigiwa magoti au kwa kukemea giza usiku. Mabadiliko husababishwa na kutekelezwa.

Tukijifunza kwenye kampeni ya Obama utaona kuwa Wamarekani hawakuombea tu kuwa kiongozi mzuri au wamtakaye aje na alipojitokeza hawakukaa pembeni kuombea kuwa afanye vizuri ili hatimaye "alete mabadiliko" wanayoyataka. Wamarekani walishirikishwa katika kampeni kuanzia kuchangia fedha, muda wao, vipaji vyao n.k

Je kwanini tunafikiri sisi Tanzania tutapata mabadiliko kwa kubishana vijiweni na kwenye mitandao na kuoneshana nani anajua nini na anahusika na nini? Mabadiliko ndugu zangu hayaji kwa kunuia au kuwa "kusudio zuri" au kwa kujua ufisadi ulivyo mbaya na fisadi ni nani!!

Mabadiliko huletwa na watu waliokusudia kuleta mabadiliko hayo. Nisikilize.


Ripoti juu ya Meremeta yatoka

play
2009-07-26 Length: 19m 21s
Unaweza kupata sneak ripoti hiyo kwenye http://www.mwanakijiji.com

Password ya kufungulia Ripoti Sneek Pek: meremeta1997

Inapatikana hivi: (Tafadhali angalia masahihisho kutoka taarifa yetu ya Ijumaa) Ripoti inapatikana kwa njia ya pre-ordering (yaani order zikishatimia zote zinatolewa kwa wakati mmoja) kwa wale ambao watachangia dola 30 au shilingi elfu thelathini tu au zaidi kwa njia zifuatazo:

* Kupitia Mtandao wa http://www.mwanakijiji.com kuna kitufye cha kuchangia upande wa kulia juu(Donate Button) cha Paypal Inc., Hapo tunaweza kupokea malipo ya kadi za kibenki katika njia ya usalama wa hali ya juu na wachangiaji wote wanamakia sirini (rekodi yetu ya miaka mitatu hatujawahi kuvujisha jina la mchangiaji yeyote yule!).Kadi za Visa, MasterCard, Express zinapokelewa.

* Kwa taasisi au watumishi wa umma (VIPs) ambao kwa sababu za wazi wangependa kutojulikana wasiliana nami kwa email au Private Message na utapata maelezo ya kuwasiliana na Mwandishi wa Habari Mchunguzi wa gazeti la kiingereza la kila siku la nchini aliyepo Tanzania ambaye atapokea fedha hiyo pamoja na email yako ambayo tutakutumia nakala hiyo katika usiri mkubwa. Yeye pia anaweza kupokea kwa njia ya Western Union kwa wale ambao wangependa kutumia njia hiyo.

* Kwa mtu mwingine yeyote tuma fedha kwa njia yarecharge vouchers kwenda namba: 0713444649. Vouchers ziwe ni za tiGO, Zain au Zantel.

Kama mipango yote itakwenda ilivyo, basi tunatarajia kutuma nakala hizo 100 siku ya Jumatano wiki ijayo kwa wale waliochangia. Hivyo ina maana watu wana siku tano za kukamilisha oda zao. Pamoja na ripoti hiyo, tumeambatanisha pia ripoti yetu ya 2006 juu ya “Tracing Reports of Tanzania’s role in arms trafficking”.

Oda nakala yako mapema kwani tutafanya kwa mtindo wa “aliyewahi mpe” – first come, first serve.

NB: - Email moja kwa nakala moja. - Hakuna nakala itakayotangulia mchango; na hakuna mtu atakayepata nakala kabla ya watu wengine. Watu wote watakaokuwa wamechangia watapata nakala zao Jumatano. NO EXCEPTION.


About this podcast:

KLH News

The most prominent, provocative, and premier Swahili podcast by an author and political analyst M. M. Mwanakijiji and the crew. The podcast is intended to be an instrument that facilitate positive attitudinal and mentality change among Tanzanians as they try to build a modern, vibrant, and prosperous African nation. This podcast is full of political, socio-economic opinions, news, and commentaries. The show also showcase now and then some Tanzanian music and other talents. To keep yourself in the "loop" of what is going on in Tanzania, you should subscribe to this, it'll be one of the best decisions you have made. If you find this podcast to be interesting, why don't you recommend it to other Tanzanians? It is our mission to reach as many Tanzanians as possible, alone the task will be difficult with your help however, the sky is the limit!

KLH News